WAJASIRIAMALI PEMBA WAPIGWA MSASA KATIKA KUELEKEA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI.

  • Mar 16, 2017
  • 159 Views

Wajasiriamali wa vikundi mbali mbali vya uzalishaji mali vikiwemo vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa vya SACCOS vya Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba wametakiwa kutengeza na kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango ambazo zitaweza kukidhi haja ya ushindani wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bi Rahma Ali Khamis amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Idara yake ya Ushirikiano wa kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi imekuwa ikichukua juhudi na kutumia mbinu mbali mbali za kuwajengea uwezo wajasiriamali kwa kutoa elimu ya kuzitambua fursa za kibiashara zinazopatika kwa kuwepo Mtangamano Jumuiya ya Afrika Mashariki ili waweze kujitayarisha na utengenezaji wa bidha zenye ubora zitakazo kidhi viwango vya ushindani wa Soko la pamoja la Jumuiya hiyo.

Akizungumza katika mikutano ya semina za mafunzo ya wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba inayohusiano na elimu ya Mtangamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki Bi Rahma aliwasisitiza wajasiriamali hao kutengeneza bidha zenye asili ya kizanzibari ambazo zinakuwa na nafasi kubwa katika soko la moja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa bidhaa za aina hiyo hazipatikani katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Semina hizo zilizoendeshwa na ndugu Suleiman Muhsini ambae ni afisa wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Nje ya Nchi anae shughulikia masuala ya Mtangamano wa kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ndugu Suleiman alieleza kuwa dhamira ya mafunzo hayo ni kuwaweka tayari kiushindani wajasiriamaliwa Mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba ili kufikia lengo la kunufaika na fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo. 

Aidha alianisha changamoto na fursa za soko la pamoja la Jumuiya hiyo kwa kuonyesha uwezo na mapungufu ya wajasiriamali wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika kuchangamkia fursa za soko hilo, vile vile aliainisha mbinu za kupambana na changamoto na nafasi za taasisi za Serikali na sekta binafsi katika kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya soko la pamoja.

Wakitoa michango yao wajasiriamali wa kisiwani Pemba waliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuwajengea uwezo na kuwawekea mazingira mazuri zaidi ambayo yataweza kuwashajiisha na kuwasukuma katika utengenezaji wa bidhaa bora na zenye ushindani ambazo zitakidhi mahitaji ya soko hilo na hatimae wazazniabari nao wanufaike na fursa za uwepo wa jumuiya hiyo .

Mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa kwa taasisi za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali ni miongoni mwa shughuli zinazotekelezwa na idara kupitia programu kuu ya Ushirikiano wa Kikanda, Kimataifa na Uratibu wa Zanzibar Wanaoishi Nchi za Nje ikiwa ni miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Idara hiyo katika kuwaandaa wananchi na wadau husika kuchangamkia na kuzitumia ipasavyo fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Related Articles